Habari Mpya

Chumo Yashinda Tuzo Golden Hamster

Filamu ya Chumo imeshinda tuzo za Golden Hamster katika tamasha la filamu la Northwest Projections, Washington, Marekani. Kwa maelezo zaidi kuhusu tuzo hizi tembelea wavuti ya Northwest Projections Film Festival.

Chumo yateuliwa na ZIFF

Filamu ya Chumo imechaguliwa kushiriki katika kinyang'anyiro cha tuzo za filamu za tamasha la ZIFF huko Zanzibar. Tamasha la ZIFF litajiri kuanzi June 18 hadi 26, 2011. Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea wavuti ya ZIFF.

Chumo Yateuliwa na Northwest Projections Film Festival

Filamu ya Chumo iliyoongozwa na Jordan Riber, pamoja na filamu nyingine ya makala, Mwamba Ngoma, kwa pamoja zimechaguliwa kushindania tuzo za filamu katika tamasha la filamu la Northwest Projections Film Festival, huko Marekani. Chumo inashindania tuzo ya filamu bora fupi, wakati Mwamba Ngoma inashindania tuzo ya filamu ndefu. Kwa habari zaidi tembemela wavuti ya Northwest Projections Film Festival.

Chumo Yateuliwa na Pan Africa Film Festival

Tamasha la filamu la Pan Africa limeiteua filamu ya Chumo kushindania tuzo zake huko Los Angeles, Carlifornia, katika kitengo cha filamu fupi. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa filamu hii kuoneshwa katika ardhi ya Marekani. Filamu itaoneshwa February 18, saa kumi na mbili na nusu ya jioni, Februari 20 kuanzia saa sita na nusu ya mchana. Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea PAFF Website.

Muhtasari wa Hadithi

Juma ni mvuvi maskini anayependa sana kupiga hadithi. Amina ni msichana anayependa kusikiliza hadithi zake . Wanatamani wawe pamoja, lakini baba yake Amina, Ali, anataka binti yake awe na maisha mazuri. Ali anamwona Yustus, kijana tajiri, mwenye kujituma kuwa ndiye anayefaa kuwa mchumba.

Inambidi Juma atumie nyenzo zake zote kuliokoa penzi lao, lakini ni lazima ajitoe mhanga zaidi ya alivyopatana ili afanikiwe.

Imetayarishwa Tanzania na kufadhiliwa na JHU-CCP kupitia Mfuko wa Rais wa kutokomeza Malaria na USAID. Chumo inawasilisha ujumbe wa malaria wakati wa ujauzito kupitia hadithi ya kusisimua ya wapenzi wenye bahati mbaya.

Wahusika Wakuu

Juma - Hussein Mkiety Amina - Jokate Mwegelo Yustus - Yusuph Milela Ali - Jafari Makati

...Ona Zaidi