Imetengenezwa na kufadhiliwa

Kampuni ya Uzalishaji

Media for Development International - Tanzania

Ufadhili

Johns Hopkins University Center for Communication Programs (JHUCCP), na
Mfuko wa Rais wa Kupambana na Malaria (PMI) kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID)

Wahusika na Mafundi

Mwongozaji

Jordan Riber

Watayarishaji

John and Louise Riber

Mchanganya picha

Owen Prum

Mwongozaji Msaidizi 1

Ezequiel Odhiambo

Mwongozaji Msaidizi 2

Tito Mwaipopo

Picha za sinema

John Riber
Jordan riber
Andrew Whaley
Ali Mbwana

Wahariri

Jordan Riber and Louise Riber

Sauti na Muziki

Julian Gordon Hastings

Wahusika Wakuu

Juma: Hussein Mkiety
Amina: Jokate Mwegelo
Ali: Jafari Makati
Yustus: Yusuph Milela

Maisha ya Muongozaji

Muongozaji wa ‘Chumo’ Jordan Riber amekulia Harare, Zimbabwe, ni mtoto wa kiume wa Watengeneza filamu maarufu John na Louise Riber. Akiwa amekulia katika mazingira ya vifaa vya filamu na matayarisho yake, alipata uzowefu wake wa mwanzo kama injinia wa sauti kwenye studio za MFDI huko Harare. Miaka mitano iliyopita, Jordan alihamia Tanzania na kujishughulisha zaidi katika utayarishaji na uongozaji katika filamu na radio. Hivi sasa anaishi Dar es Salaam, mtengenezaji filamu kijana mwenye mwanga wa maisha bora ya baadaye. Kilicho muhimu kwake hivi sasa ni kukua kama mtengeneza filamu, na wakati huo huo kuchangia katika kuwakuza watengeneza filamu vijana kama yeye hapa Tanzania. ‘Chumo’ ni filamu yake ya kwanza.

MUHTASARI WA HADITHI

Juma ni mvuvi maskini anayependa sana kupiga hadithi. Amina ni msichana anayependa kusikiliza hadithi zake . Wanatamani wawe pamoja, lakini baba yake Amina, Ali, anataka binti yake awe na maisha mazuri. Ali anamwona Yustus, kijana tajiri, mwenye kujituma kuwa ndiye anayefaa kuwa mchumba.

Inambidi Juma atumie nyenzo zake zote kuliokoa penzi lao, lakini ni lazima ajitoe mhanga zaidi ya alivyopatana ili afanikiwe.

Imetayarishwa Tanzania na kufadhiliwa na JHU-CCP kupitia Mfuko wa Rais wa kutokomeza Malaria na USAID. Chumo inawasilisha ujumbe wa malaria wakati wa ujauzito kupitia hadithi ya kusisimua ya wapenzi wenye bahati mbaya.