Muziki Toka Filamu ya Chumo

Video ya Jagwa

Filamu ya Chumo iliona ni vyema kuwa na muziki wa mchiriku ambao ungepigwa moja kwa moja katika kijiji cha kina Juma. Kikundi cha muziki cha Jangwa kutoka Mwananyamala, Dar es Salaam, kilitunga "Mwana wa Kitwana", na kuucheza wimbo huo katika filamu.

 

Ashimba

Mwishoni mwa mwaka 2010, Ashimba akishirikiana na muongozaji wa Chumo, Jordan Riber pamoja na mtaalamu wa muziki, Julian Gordon-Hastings na kufanikiwa kutengeneza nyimbo mbili kwa ajili ya filamu.

"Tulifahamu kwamba tulihitaji kitu ambacho kitakuwa rahisi kusikiliza, kitu chenye maajabu ndani yake, aina ya muziki ambao tungeweza kuutumia katika sehemu kadhaa katika filamu," anasema Jordan, "na kila tulipotazama tuliona kwamba Ashimba ndio hasa ambaye angefanikisha hilo. Na hata alipokuja kurekodi kila kitu kilikwenda bila kukwama. Ilipendeza sana kumtazama. Wimbo wa kwanza ulikuwa mzuri mno, tukashawishika kunya na wapili."

Bofya hapo chini kusikiliza nyimbo cha Chumo na Chereko zilizorekodiwa na Juliana Gordon-Hastings na kuchezwa na Ashimba.

Chumo:
Chereko:

Muhtasari wa Hadithi

Juma ni mvuvi maskini anayependa sana kupiga hadithi. Amina ni msichana anayependa kusikiliza hadithi zake . Wanatamani wawe pamoja, lakini baba yake Amina, Ali, anataka binti yake awe na maisha mazuri. Ali anamwona Yustus, kijana tajiri, mwenye kujituma kuwa ndiye anayefaa kuwa mchumba.

Inambidi Juma atumie nyenzo zake zote kuliokoa penzi lao, lakini ni lazima ajitoe mhanga zaidi ya alivyopatana ili afanikiwe.

Imetayarishwa Tanzania na kufadhiliwa na JHU-CCP kupitia Mfuko wa Rais wa kutokomeza Malaria na USAID. Chumo inawasilisha ujumbe wa malaria wakati wa ujauzito kupitia hadithi ya kusisimua ya wapenzi wenye bahati mbaya.

WAHUSIKA WAKUU

Juma - Hussein Mkiety Amina - Jokate Mwegelo Yustus - Yusuph Milela Ali - Jafari Makati

...Ona Zaidi